• [button style=”info” href=”http://www.rsa.or.tz/fomu-ya-maoni/”]FOMU YA MAONI[/button]

RSA washiriki maadhimisho ya miaka 100 ya skauti nchini

– Watoa mafunzo kuhusu usalama barabarani.
– Waelezea historia ya RSA Tanzania na inapokwenda
– Watakiwa ‘kuambukiza’ watoto utamaduni wa kuheshimu barabara

Ukuaji wa RSA Tanzania kama taasisi, pamoja na kukubalika kwa shughuli zake, vinaendelea kujionyesha kila siku, kwa taasisi hii kupokea mialiko ya kushiriki shughuli mbalimbali za uelimishaji katika matukio mbalimbali yakiwemo yale ya kitaifa.

Katika tukio la hivi karibuni, RSA ilipewa mwaliko wa kushiriki kwa kutoa mafunzo katika maadhimisho ya miaka 100 ya skauti duniani, tukio ambalo kitaifa limefanyika mkoani Dodoma, katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), na kuhudhuriwa na skauti wa rika mbalimbali wapatao 3500, toka mikoa yote ya Tanzania.

Mwaliko huo ambao ulisainiwa na Skauti Mkuu nchini, mhe. Mwantumu Mahiza, uliuelekeza mtandao wa mabalozi wa usalama barabarani kuhudhuria sherehe hizo za wiki moja kwa minajili ya kuwapatia skauti hao, elimu kuhusu masuala mbalimbali ya usalama barabarani, ili kuwawezesha kwenda kusambaza elimu hiyo kwa watu wengi zaidi pindi wakirejea makwao baada ya kambi.

Kwakuwa RSA imekuwa ikishirikiana kwa karibu na mamlaka mbalimbali zinazohusika na sekta ya usafirishaji, iliwasiliana na ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, mkoa wa Dodoma (RTO), ambapo wapatiwa mmoja wa askari walio upande wa uelimishaji, ili kusaidiana katika kufanikisha jukumu hilo, pamoja na kuzidi kuimarisha mahusiano baina ya pande hizi mbili.

Mafunzo hayo, yakaendeshwa na koplo Martin Mangu, toka ofisi ya RTO dodoma, Marlin Komba na Ramadhani Msangi, ambao ni watendaji toka RSA Taifa na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Wawili hawa wakapata nafasi ya kuwasilisha mada kadhaa ambazo zilikuwa na lengo la kuwawezesha skauti hao kuweza kuzitumua, katika uelimishaji wao au pale wanapokuwa wamekumbwa na shida wawapo safarini.

Miongoni mwa mada zilizowasilishwa ilikuwa ni maana na aina za barabara, matumizi sahihi ya barabara, makundi ya watumiaji wa barabara, wajibu wa watumiaji mbalimbali wa barabara hususan watembea kwa miguu na waendesha baiskeli pamoja na maana na sababu za ajali.

Aidha, waliweza pia kuelezwa kuhusu RSA, ilipotoka ilipo na inakoelekea, huku wakipatiwa mawasiliano ya namba za simu ambazo wataweza kuzitumia kujiunga na mtandao, pindi watakaporejea katika mikoa yao.

Skauti Mkuu Bibi Mwantumu Mahiza, pamoja na Kamishna wa Skauti nchini, Mhe. Abdulkarim Shah, walieleza kufurahishwa kwao na ushiriki wa RSA pamoja na elimu waliyoitoa, huku wakihimiza taasisi kuangalia uwezekano wa kuhakikisha inajielekeza maeneo ya kandokando ya miji kwa ajili ya uelimishaji, sanjari na kutilia mkazo kuelimisha watoto, ili waweze kukua na utamaduni wa kuheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani

Maadhimisho ya miaka 100 ya skauti, yalizinduliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, huku yakitarajiwa kuhitimishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mabadiliko katika Jeshi yanatuacha salama

Uongozi wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Barabarani nchini (RSA), umeeleza kuridhishwa kwake na mabadiliko ya kimaboresho yanayoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi nchini, huku uongozi huo ukisema hauna mashaka na mabadiliko hayo, kwakuwa yanauacha ukiwa salama.

Uongozi huo, umelazimika kutoa tamko hilo, kufuatia wasiwasi uliokuwa umeibuka miongoni mwa wanachama wake, ambao walikuwa wakihoji juu ya hatma ya RSA Tanzania, baada ya aliyekuwa mlezi mwanzilishi wa mtandao huo, DCP Mohammed Mpinga, kupata uhamisho wa kikazi, ambapo hivi sasa anakuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.

Ifahamike kuwa, kwa mujibu wa katiba ya RSA Tanzania, mlezi wake mkuu kitaifa anakuwa ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, huku katika ngazi ya mikoa, makamanda wa mikoa wa kikosi hicho, wakiwa ndio walezi wake.

Aidha, hivi karibuni, Inspekta Jenerali wa Polisi nchini, alifanya mabadiliko kadhaa yenye lengo la kuimarisha utendaji wa Jeshi hilo, ambapo katika mabadiliko hayo, DCP Mpinga, aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, amepelekwa kuwa Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mbeya, huku nafasi yake ikichukuliwa na aliyekuwa msaidizi wake, SACP Fortunatus Musilimu.

Kufuatia mabadiliko hayo, SACP Musilimu, anatarajiwa kukabidhiwa rasmi mikoba ya ulezi wa RSA Tanzania, toka kwa mtangulizi wake, ambapo uongozi wa RSA, umeeleza kuwa, mabadiliko hayo hayatakuwa na athari yoyote katika uendeshaji na usimamizi wa shughuli za RSA, kwani mlezi anayeingia, amekuwa akiifahamu RSA, pamoja na kushiriki katika shughuli zake kadhaa, tangu kuanzishwa kwake.

“Kamanda Musilimu, tumekuwa naye akiwa msaidizi wa mlezi mwanzilishi. Ameshirikiana nasi katika shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maadhimisho ya Siku ya Mabalozi, iliyofanyika Dodoma hivi karibuni, kwahiyo ni mtu ambaye tunaamini atatusimamia vizuri kuendeleza malengo yetu ya kulisaidia Jeshi la Polisi, kuweza kupungiza matukio ya ajali nchini” imeeleza sehemu ya taarifa ya uongozi wa RSA.

Kamanda Musilimu, ataendelea kusaidiwa majukumu ya ulezi wa RSA, na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Barabara toka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), ndugu Johansen Kahatano.

Katika hatua nyingine, sherehe rasmi za kumuaga DCP Mpinga kama mlezi wa RSA pamoja na kumkaribisha mlezi mpya SACP Musilimu, zinatarajiwa kufanyika mkoani Kilimanjaro, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani kitaifa, maadhimisho ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Healthy Waffle Recipe

Healthy Waffle Recipe

Morbi quam libero, accumsan at vestibulum sed, semper id risus. Donec dapibus volutpat facilisis. Donec eu urna id nulla tincidunt euismod id ac mi. Pellentesque feugiat mi sed ligula blandit semper. Vivamus varius, tellus quis fermentum interdum, mauris quam rutrum arcu, id ultricies risus dolor nec metus. Aenean elit leo, egestas at dignissim quis, facilisis at dolor. Suspendisse potenti.
Read more

Why Breakfast is Important

Ut luctus lacus elit. In ligula augue, pulvinar eget dignissim a, blandit eget dolor. Cras eleifend urna eget diam tempor vel luctus ligula eleifend. Suspendisse eros massa, suscipit vitae mollis eget, mattis vel elit. Nunc ultrices porttitor vehicula. Nulla ligula tortor, mollis a faucibus ut, tincidunt eget eros. Quisque id dui dolor, sit amet viverra mi. Maecenas accumsan, est sed varius viverra, purus nisl fermentum nunc, id bibendum erat mi vulputate tellus.
Read more

Online Food Shopping?

Online Food Shopping?

Morbi venenatis quam ac metus tempor et porttitor ligula suscipit. Ut tellus ligula, semper ut viverra vitae, euismod sed lacus. Mauris dictum scelerisque ante, in iaculis felis facilisis sed. Sed ultricies cursus enim, at varius nisi eleifend non. Donec magna turpis, porttitor vel laoreet ac, viverra sit amet eros. Vestibulum ante ipsum primis in faucibus orci luctus et ultrices posuere cubilia Curae; Sed odio velit, tempor vel tincidunt non, adipiscing ut turpis.
Read more

Too Much Medication?

Too Much Medication?

Vestibulum a eros a dui efficitur varius. Proin eu dapibus massa. Donec vulputate consequat sapien, vel vestibulum sapien venenatis nec. Mauris in ornare metus. Pellentesque ultrices hendrerit ullamcorper. Vivamus in maximus libero. Integer eu bibendum risus, vel venenatis velit. Nullam commodo leo et mauris volutpat, eget gravida ex tincidunt. Donec aliquet sapien vel tempor faucibus. Nullam non lacus nec ex aliquam luctus. Suspendisse quam erat, tristique non vulputate sit amet, pellentesque vitae urna.
Read more

We Offer New Therapy

We Offer New Therapy

Vestibulum a eros a dui efficitur varius. Proin eu dapibus massa. Donec vulputate consequat sapien, vel vestibulum sapien venenatis nec. Mauris in ornare metus. Pellentesque ultrices hendrerit ullamcorper. Vivamus in maximus libero. Integer eu bibendum risus, vel venenatis velit. Nullam commodo leo et mauris volutpat, eget gravida ex tincidunt. Donec aliquet sapien vel tempor faucibus.
Read more